Isaiah 40:3-5


3 aSauti ya mtu aliaye:
“Itengenezeni jangwani njia ya Bwana,
nyoosheni njia kuu nyikani
kwa ajili ya Mungu wetu.
4 bKila bonde litainuliwa,
kila mlima na kilima kitashushwa;
penye mabonde patanyooshwa,
napo palipoparuza patasawazishwa.
5 cUtukufu wa Bwana utafunuliwa,
nao wanadamu wote watauona pamoja.
Kwa maana kinywa cha Bwana kimenena.”
Copyright information for SwhNEN